Wakala wa Vipimo ina majukumu yafuatayo:
1:Kumlinda mlaji katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya kupitia matumizi ya vipimo sahihi;
2:Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya;
3:Kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wanaojihusisha na utengenezaji, uundaji, na uingizaji wa vipimo mbalimbali katika Biashara, Usalama, Mazingira na Afya;
4:Kuwa kiungo kati ya Taifa letu na taasisi za kikanda na Kimataifa katika masuala ya Vipimo (Legal Metrology);
5:Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini kama standards za vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa;
6:Kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa (Net quantity & labeling);
7:Kutoaelimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau.