Wanolewa utekelezaji Mkataba wa Huduma kwa Mteja

MOROGORO-Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Utumishi imetoa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutoka ofisi za wakuu wa mikoa.
Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Bi. Beatrice Kimoleta akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakati akifungua mafunzo hayo mjini Morogoro yanayotolewa katika na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).

Akifungua mafunzo hayo mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa, Beatrice Kimoleta, amewataka washiriki kutumia maarifa yatakayopatikana ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na uwajibikaji zaidi.
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo hayo mjini Morogoro yanayotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Mkufunzi wa Mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Noah Mkasanga akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo hayo, yanayotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Raslimaliwatu Mkoa wa Singida, Bw. Steven Pancras, akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta kufungua mafunzo hayo mjini Morogoro yanayotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakimsikiliza Mwenyekiti wa mafunzo hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Utawala na Raslimaliwatu Mkoa wa Singida Bw. Steven Pancras kabla hajamkaribisha Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta kufungua mafunzo hayo yanayotolewa mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, mara baada ya kufungua mafunzo hayo mjini Morogoro yanayotolewa katika na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).

Amesisitiza kuwa mikataba hiyo itawawezesha wananchi kupata huduma bora kwa wakati, huku akiwataka maafisa wa mawasiliano kuhakikisha elimu kuhusu utekelezaji wake inawafikia wananchi kupitia mikutano na semina mbalimbali.

Kaimu Katibu Tawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Elihuruma Nyella amesema wamepokea maelekezo ya Mkurugenzi Kimoleta, hivyo watahakikisha wananchi wanapata huduma bora kama zitakavyoanishwa kwenye mikataba ya huduma kwa mteja ya ofisi za wakuu wa mikoa nchini.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Elihuruma Nyella akiahidi kutekeleza maelekezo ya Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta, mara baada ya mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kwa watendaji wa ofisi za wakuu wa mikoa yanayotolewa katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bw. Ambwene Mwaifuge akiahidi kutekeleza maelekezo ya Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta, mara baada ya mkurugenzi huyo kufungua mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kwa watendaji wa ofisi za wakuu wa mikoa yanayotolewa katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ambwene Mwaifuge amesema kuwa, Maofisa Habari wanalo jukumu la kuitangaza mikataba ya huduma kwa wateja kupitia mikutano ya hadhara, mikutano ya dini na semina mbalimbali zitakazofanyika ndani ya mikoa ili mikataba hiyo itumike ipasavyo katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Beatrice Kimoleta akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, mara baada ya kufungua mafunzo hayo mjini Morogoro yanayotolewa katika na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).

Mafunzo haya ya siku nne yanatarajiwa kuwajengea uwezo washiriki katika kuandaa mikataba ya huduma kwa wateja, hatua inayolenga kuboresha huduma za umma nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news