Wasanii kutoka Brazili kutumbuiza Zanzibar

ZANZIBAR-Kwa mara ya kwanza, Ubalozi wa Brazil katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kushirikiana na Gavana wa Jimbo la Bahia nchini Brazili na Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA) wanajivunia kuwaleta hapa Zanzibar Wasanii wakubwa kutoka nchini Brazil walioshinda tuzo nyingi duniani, kuja kwenye onyesho Maalum na la kipekee la mabadilishano Sanaa na Utamaduni.

Tukio hili inawashirikisha Wanamuziki wawili wanaotambulika kimataifa Mwanafalsafa mahiri bw. Ivan Sacerdote, na Felipe Guedes, mshindi wa tuzo ya upigaji gitaa kutumbuiza pamoja na wanamuziki mahiri kutoka Zanzibar wa Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA).

Tukio hili la kipekee litafanyika katika Hoteli ya kifahari ya Maru Maru siku ya Jumapili, tarehe 26 Januari 2025, kuanzia 12:30 jioni hadi 04:00 usiku.

DCMA inaahidi kuwa na jioni maalum yenye kusisimua ya mchanganyiko wa muziki wa ubora na kitamaduni.

Ushirikiano huo unalenga kusherehekea ukuzaji wa muziki wa asili wa Zanzibar huku ukiangazia utunzaji wa urithi tajiri wa muziki wa Zanzibar na wa eneo la Bahia nchini Brazili, na kukuza uhusiano wa kutembeleana na kukaribisha utalii kati ya mataifa hayo mawili. Ujio huu ni muondelezo wa mahusiano ya nchi mbili na kufuatia ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Brazil mwaka jana mwezi wa November 2024.

Maarufu wa umahiri wao kimataifa, Ivan Sacerdote na Felipe Guedes watachanganya ubunifu wao, mitindo ya sauti za kusisimua, za kihistoria ya Brazil, na kujenga mandhar murua ya muziki.

Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA), kilichopo katikati ya Mji Mkongwe, ni Taasisi pekee inayotoa taaluma ya muziki wa Asili na wa kisasa Zanzibar na Ukanda wa Afrika Mashariki.

Taasisi inayojitolea kufundisha, kuhifadhi, na kukuza tamaduni tajiri za muziki za mwambao wa Bahari Hindi.

DCMA ilianzishwa mwaka 2001 na kuwa mstari wa mbele katika kukuza vipaji mbalimbali na kulinda Urithi wa kitamaduni wa Zanzibar hususan Muziki wa Taarab, Kidumbaki, Ngoma mbalimbali za wazawa na wasanii wengine. Chuo kinatoa elimu bora ya muziki kwa wanafunzi wa kila rika na asili mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news