DAR-Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili Husna Gulam (3) na Mahdi Mohamed (4) walioibiwa na dada wa kazi kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji nyumbani kwao Tandika jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watoto hao wamepatikana Januari 14, 2025 nyumbani kwa mganga huyo Abdulkarim Shariff (43), Kimara Baruti jijini Dar es Salaam, ambapo walipelekwa Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na hawajakutwa na tatizo lolote.