Waziri aipongeza BoT kwa kushiriki Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar

ZANZIBAR-Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Chamanangwa, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katika ziara hiyo, Waziri Shaaban alipata nafasi ya kujifunza kuhusu majukumu mbalimbali ya Benki Kuu ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na jukumu lake katika kusimamia sera za fedha na kuhakikisha uthabiti wa sekta ya fedha nchini.

Aidha, alielezwa kwa kina kuhusu fursa za uwekezaji katika dhamana za serikali, ambazo ni njia salama na yenye faida kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.

Pia, ameipongeza BoT kwa ushiriki wake katika maonesho hayo kama sehemu ya jitihada zake za kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi kuhusu masuala ya kifedha.
Alieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa sababu inawawezesha wananchi kuelewa si tu majukumu ya msingi ya Benki Kuu, bali pia nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zinazotolewa na BoT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news