Waziri Bashungwa awasili makao makuu ya Jeshi la Polisi

DODOMA-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa leo tarehe 22 Januari 2025 amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo.
Katika ziara hiyo ya kwanza ya Kikazi katika Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri Bashungwa amepokelewa kwa salamu ya gwaride la heshima (Mounted Guard).

Pamoja na mambo mengine, Waziri Bashungwa atafanya kikao na kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali na Watumishi wengine wa Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news