Waziri Dkt.Nchemba afungua mafunzo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)

NA BENNY MWAIPAJA

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amefungua mafunzo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu Usimamizi wa Fedha za Umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) na kuipongeza Kamati hiyo kwa kutekeleza kikamilifu jukumu lake la msingi la usimamizi (oversight) wa fedha za umma na kukuza utawala bora katika nchi hatua ambayo imeendelea kuisadia Serikali kuboresha maandalizi ya hesabu za Serikali, kuimarisha mifumo ya kielekroniki ya usimamizi wa fedha za umma, na kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa bajeti inayoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila Mwaka.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, akizungumza jambo wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kufungua mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati akifungua mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Josephat Hasunga, akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati hiyo yaliyofunguliwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, na kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (mwenye tai ya Bendera ya Tanzania), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), baada ya kufungua mafunzo maalum ya Siku tano (5) kwa Kamati hiyo, yanayohusu usimamizi wa fedha za umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, yanayofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha).

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya PAC, Mheshimiwa Josephat Hasunga, ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuandaa mafunzo hayo kwa Wajumbe wa Kamati yake na kwamba mafunzo hayo yatawajengea uwezo zaidi wa kuelewa namna Serikali kupitia Wizara ya Fedha inavyotekeleza majukumu yake kikamilifu katika usimamizi wa Fedha za umma zinazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii na kukuza uchumi wa nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news