Waziri Dkt.Nchemba akaribisha wawekezaji kutoka Japan kuwekeza Tanzania

NA BENNY MWAIPAJA
WF Dodoma

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa wito kwa Kampuni za Japan kuwekeza nchini Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji kwa faida ya pande zote mbili.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati) na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja naNaibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa tano kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa nne kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli (wa tatu kulia), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi (wa nne kushoto) na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo Jijini Dodoma wakati akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe.Yasushi Misawa, ambapo pamoja na mambo mengine, alimhakikishia pia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili.

Alisisitiza kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo sekta ya kilimo itakayoiwezesha Tanzania kuwa ghala la chakula lakini pia uwekezaji katika miundombinu ikiwemo uendeshaji wa Reli ya Kisasa SGR.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), akiongoza kikao chake na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (hayupo pichani) jijini Dodoma, ambapo alitoa wito kwa Kampuni za Japan kuwekeza nchini Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji kwa faida ya pande zote mbili, na kumhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa pili kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Sera anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Masuala ya Kodi, Bw. Juma Mkabakuli (wa tatu kulia), na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Aidha, katika mazungumzo yao, Dkt. Nchemba aliishukuru Japan kwa uwekezaji mkubwa uliochangia maendeleo ya nchi kupitia miradi mbalimbali iliyofadhiliwa na nchi hiyo katika sekta za kilimo, afya, nishati, na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Barabara ya mzunguko katika jiji la Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (hayupo pichani) jijini Dodoma, ambapo alitoa wito kwa Kampuni za Japan kuwekeza nchini Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji kwa faida ya pande zote mbili, na kumhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili.

“Katika kipindi chako pekee, tumeshuhudia Tanzania na Japan zikisaini mikataba ya mikopo nafuu yenye thamani ya yen ya Japan bilioni 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 151 pamoja na msaada wa yen bilioni 5.5, sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 83. Tunakushukuru sana na tunakuomba uendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza muda wako,"alisisitiza Dkt. Nchemba.
Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (kushoto), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma, ambapo alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake umedumu kwa zaidi ya miaka 60 ambapo katika kipindi hicho, Japan imesaidia utekelezaji wa zaidi ya miradi 360 ya kijamii na kiuchumi ikiwemo miradi ya sekta ya nishati ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa njia ya umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga, ujenzi wa mradi wa umeme unaounganisha Tanzania na Kenya pamoja na mpango unaoendelea kati ya Tanzania na Japan kupitia Wizara ya Nishati wa kujenga mradi wa umeme wa joto ardhi. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi.

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa, aliyeambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Ara Hitoshi, alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake umedumu kwa zaidi ya miaka 60 ambapo katika kipindi hicho, Japan imesaidia utekelezaji wa zaidi ya miradi 360 ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Dkt. Nchemba alitoa wito kwa Kampuni za Japan kuwekeza nchini Tanzania ili kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji kwa faida ya pande zote mbili, na kumhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania na Japan zitaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kiuchumi na kijamii kwa faida ya nchi hizo mbili.

Alibainisha kuwa baadhi ya miradi hiyo iko katika sekta ya nishati ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa njia ya umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga, ujenzi wa mradi wa umeme unaounganisha Tanzania na Kenya pamoja na mpango unaoendelea kati ya Tanzania na Japan kupitia Wizara ya Nishati wa kujenga mradi wa umeme wa joto ardhi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akimkabidhi zawadi ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini, Balozi wa Japan nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano na namna ya kutumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini kwa faida ya pande zote mbili.

Katika mazungumzo yao ambayo yalihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, viongozi hao walijadili fursa mbalimbali za maendeleo katika sekta za kilimo, afya, miundombinu, na kukuza uchumi na maendeleo ya nchi kupitia ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news