Waziri Dkt.Nchemba ashiriki mkutano wa Kamati ya Barabara Mkoa wa Arusha

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameshiriki mkutano wa Kamati ya Barabara ya Mkoa wa Arusha na kuahidi kuwa Serikali itaongeza kasi ya mtiririko wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya Barabara nchini ukiwemo mkoa wa Arusha hususan kwenye miradi ambayo iko katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji ili kuchochea kasi ya uchukuzi wa bidhaa na watu, hatua ambayo amesema itachangia ukuaji wa kipato kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ahadi hiyo inafuatia maombi maalumu yaliyowasilishwa katika Mkutano huo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ambaye alisisitiza umuhimu wa Serikali kuupa mkoa huo kipaumbele katika kuboresha miundombinu yake ya Barabara kutokana na umuhimu wake katika kuchangia mapato ya Serikali hususan katika sekta ya utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news