ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), akiambatana na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, walipomtembelea Ofisini kwake jijini Arusha, walipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba na Mhe. Ulega, walishiriki mkutano maalum wa Kamati ya Barabara ya Mkoa wa Arusha uliowashirikisha wadau wengine mbalimbali wakiwemo wabunge wa mkoa huo, ambapo walijadili namna va upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya Barabara mkoani Arusha ambao ni mkoa wa kitalii na unachangia wa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kutokana na mapato yanayotokana na sekta mbalimbali za uzalishaji hususan utalii.
Tags
Abdallah Ulega
Arusha Region
Dr Mwigulu Lameck Nchemba
Habari
Paul Makonda
Wizara ya Fedha Tanzania