DAR-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi Kabudi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027 kwani mashindano haya yataipa heshima nchi yetu kimataifa na Sekta ya Michezo kwa ujumla.
Prof. Kabudi ameyasema hayo Januari 4, 2025 alipozuru kukagua miundombinu ya viwanja hivyo vya Gymkana, Major general Isamuyo, na uwanja wa Law School ambapo amesema kuwa, asilimia kubwa ya ujenzi huo umekamilika na kuagiza machache yaliyobaki kutimizwa kwa wakati.
Waziri Kabudi amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa viwanja vya Mazoezi ya michuano ya CHAN vilivyopo jijini Dar es Salaam huku akiwataka SUMA JKT kuhakikisha kazi hiyo inamalizika kwa wakati.