DAR-Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi amepokea taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili ya maandalizi ya vazi hilo.
Waziri Kabudi amesema mchakato wa vazi la Taifa umeanza kuwa na mafanikio kutokana na jitihada zilizofikiwa kwa sasa ambapo kamati imewasilisha taarifa maalumu ya mapendekezo ya aina ya michoro ya vazi la Taifa kwa Wizara yake.