Waziri Kabudi ataka wanahabari kuwekeza katika teknolojia ya Akili Unde (AI)

DAR-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amewataka wahabari nchini kuwekeza kwenye teknolojia mpya ya Akili Mnemba au Akili Unde (Artificial Intelligence -AI) huku akisema teknolojia hiyo sio tishio kwa wanahabari bali ni zana ya kurahisisha, kuboresha utendaji kazi.
Prof. Kabudi amesema hayo leo akiwa Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Barabara ya Mandela, Tazara Dar es Salaam, alipoanza rasmi ziara ya kutembelea vyombo vya habari nchini tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan Desemba 08, 2024.
“Jukumu letu kubwa Watanzania na Waafrika kuhakikisha tunawekeza kwenye utengenezaji wa maudhui ‘content creation’ mengi kuhusu nchi zetu kwakuwa AI haizalishi taarifa bali huchukua taarifa kutoka vyanzo tofauti,” amesema Prof. Kabudi.

Katika hatua nyingine, amewataka wanahabari nchini kutabahari katika tasnia yao, kujikita katika kujenga uelewa, na kuondokana na tabia za uvivu kwani tasnia hiyo ni muhimu katika kuikosoa jamii, kuijenga, kutunza utamaduni, kutangaza mambo mazuri ya nchi na serikali pia kuionesha fursa mbalimbali kwaajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
“Tunahitaji waandishi wa aina hiyo, wanaoandika kwa maki na uketo,” amesema Waziri Kabudi akielezea umuhimu wa wanahabari kutabahari ‘specialization’ ili kuwa na habari za kina, zenye tija kwa taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news