DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal aliyefika katika ofisi za Wizara Dar es Salaam kutoa shukrani na kuaga akiwa anaelekea ukingoni mwa kuhudumia nchini Tanzania.

Waziri Kombo ameishukuru Algeria kwa ushirikiano mzuri wa kimaendeleo na kuahidi kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Algeria.
Kwa upande wake Balozi Djellal ameshukuru kwa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano iliyofanyika mwaka 2023.