DAR-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa Ubalozi wa Marekani nchini na kuahidi kumpatia ushirikiano wa karibu Balozi ajaye katika utekelezaji wa majukumu yake awapo Tanzania pamoja na kuangazia maeneo ya kuongeza wigo wa ushirikiano kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Waziri Kombo amemshukuru Balozi Battle kwa ushirikiano mzuri kati ya wizara na ubalozi katika kipindi chote cha uongozi wake pamoja na kufanya kazi kwa karibu na sekta na wizara mbalimbali za kimaendeleo nchini.
Aidha, ametumia fursa hii kutoa salamu za pole kwa msiba wa Rais Mstaafu wa Marekani, Hayati Jimmy Carter aliyefariki Dunia Desemba 29, 2024.

