DODOMA-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda tarehe 15 Januari 2025, Dodoma amekutana na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwa lengo la kujadili ushirikiano kati ya wizara na jumuiya hiyo.

Aidha, Prof. Mkenda amewataka wanafunzi kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa sera mpya ya elimu mnamo 31, Januari 2025 huku akibainisha kuwa maoni yao ni muhimu kwa ustawi wa mfumo wa elimu nchini.
Kwa upande wake, Rais wa TAHLISO, Bi. Maria John Thomas, amemshukuru Waziri Mkenda kwa kukubali kukutana nao, akisema kikao hicho ni hatua muhimu katika kutatua changamoto za wanafunzi wa elimu ya juu hivyo viongozi hao wa TAHLISO wameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara kuboresha mazingira ya elimu ya juu nchini.