Waziri Mkuu ataja sekta zilizochagiza kuimarisha uchumi utekelezaji wa ilani

NA GODFREY NNKO

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema,Serikali imeimarisha uchumi kupitia uwekezaji katika nishati, maji, afya, elimu, na usafirishaji.
Amesema, kiwango halisi cha ukuaji wa Pato la Taifa kimeongezeka kutoka asilimia 4.8 mwaka 2020 hadi asilimia 5.1 mwaka 2023 na kinakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024.

Majaliwa ameyasema hayo Januari 19,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi Desemba,2024.

Ni mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Pia amesema, Serikali imedhibiti mfumuko wa bei hadi asilimia 3 mwaka 2024 kutoka asilimia 3.1 mwaka 2020.
"Mapato ya ndani yaliongezeka kufikia shilingi trilioni 13.54 mwaka 2024 kutoka shilingi trilioni 8.1 mwaka 2020.

"Idadi ya walipa kodi iliongezeka hadi milioni 6.4, na Serikali imeondoa kodi zisizo na tija ili kuchochea maendeleo."

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Serikali imeendelea kupambana na umaskini kwa kusimamia programu mbalimbali ili kuinua ubora wa maisha.

"Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani, mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwemo kutoa huduma za TASAF kwa kaya za walengwa 1,357,965 katika vijiji, mitaa na shehia 17,260 Tanzania Bara na Zanzibar.
"Kutekeleza miradi 17,421 ya sekta za afya, elimu na maji na kutoa ajira za muda kwa kaya za walengwa 662,374 Tanzania Bara na Zanzibar."

Mafanikio mengine amesema ni kutoa mikopo isiyo na riba ya shilingi bilioni 240.9 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu.

Sambamba na jutoa elimu ya ujasiliamali kupitia programu maalum kwa vijana 164,443 waliomaliza taasisi za elimu ya juu na kati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news