Waziri Mkuu awasili Msumbiji kumwakilisha Rais Dkt.Samia uapisho wa Rais mteule Daniel Chapo

MAPUTO-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo, Daniel Chapo utakaofanyika kesho Januari 15, 2025.
Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, 2024.
Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.
Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa Independence (Uhuru) jijini Maputo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news