KAMPALA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2025 amewasili Kampala nchini Uganda ambapo kesho Januari 11, 2025 atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano kuhusu Mpango wa Kilimo Afrika utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort and Conference Centre Munyonyo. Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Nchi anayeshugulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda, Fredrick Bwino, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa, Balozi wa Uganda nchini, Kanali Mstaafu, Fredy Mwesigye.