WAZIRI MKUU KUZINDUA KANZIDATA NA MFUMO WA TAARIFA ZA WENYE ULEMAVU

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 25 2025 atazindua Kanzidata na Mfumo wa Taarifa za Watu Wenye Ulemavu Unaotokana Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mfumo huo utawezesha wadau wa maendeleo, na watunga sera katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu nchini.
Pia, Takwimu zilizoandaliwa zinatoa taarifa za msingi ikiwemo idadi ya watu wenye ulemavu kwa jinsi na umri, aina ya ulemavu, kiwango cha elimu na aina ya shughuli za kiuchumi wanazojishughulisha nazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news