Waziri Mkuu wa Uganda awasili nchini

DAR-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Robinah Nabbanja, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari 2025.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Nabbanja amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi.
Mheshimiwa Nabbanja yuko nchini kumuwakilisha Rais wa Uganda katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ambao unawakutanisha Viongozi wa Afrika, wadau wa sekta ya nishati, na washirika wa maendeleo.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika na kuhakikisha nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika inapatikana kwa watu milioni 300 ifikapo mwaka 2030.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news