DODOMA-Wizara ya Afya Tanzania imesema, imepokea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera ambapo kufuatia tetesi hizo imechukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo kutuma timu ya wataalamu, kufanya uchunguzi wa suala hilo, kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara.
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema,hadi Januari 15, 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibisha uwepo wa virusi vya Marburg.
“Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi pamoja na Jumuiya ya Kimataifa likiwemo Shirika la Afya Duniani (World Health Organisation-WHO) kuwa, imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na itaendelea kutoa taarifa zaidi;