DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndg. Methusela Ntonda ametembelea maeneo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika yaliyopo Wilaya ya Kongwa Dodoma na Kata ya Mazimbu Morogoro mjini.
Maeneo hayo ni ambayo yalitumika na mashujaa wa nchi za Kusini mwa Afrika (Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia na Angola) ambao walipiga kambi maeneo mbali mbali hapa nchini kipindi cha kujikomboa kutoka mikono ya wakoloni.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua meneo hayo ili yaweze kuendelezwa kwa kuwekewa mikakati ya kuyaboresha na kuyafanya yawe ya kitalii ili yaweze kuongeza mapato ya Serikali.