DAR-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeshiriki kikao cha awali cha kujadili juu ya uanzishwaji wa Makumbusho ya Taifa ya kuwaenzi Wanawake Mashujaa walioshiriki katika Harakati za Uhuru na Ukombozi wa Tanganyika na Zanzibar.
Kikao hicho ambacho kimefanyika jijini Dar es Salaam Januari 22, 2025 kimeongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Ndg. Mfaume Said na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Makumbusho ya Taifa pamoja na Women Fund Tanzania Trust.
Sambamba na hilo, wanawake walioacha alama katika nafasi mbalimbali za utumishi wa Umma watajumuishwa kwenye makumbusho hiyo.