NA DIRAMAKINI
MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (Yanga SC) ya jijini Dar es Salaam wamefufua matumaini ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Yanga SC ambayo awali ilikuwa imeanza kukatiwa tamaa, matumaini yamerejea leo Januari 4,2025 kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.
Mtanange huo umepigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza Alioune Badara Faty aliiwezesha TP Mazembe kurekodi bao la kwanza lwa penalti.
Bao hilo ambalo lilidumu kwa dakika kadhaa lilisawazishwa na Clement Mzize dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza.
Miamba hiyo miwili ya soka barani Afrika ilienda mapumziko ikiwa na bao moja kwa moja. Katika kipindi cha pili, Stephanie Azi Ki dakika ya 56 aliongeza bao la pili kwa mwajiri wake.
Clement Mzize dakika ya 60 alirejea tena kufunga mahesabu ya baada ya kufunga bao safi ambalo limewezesha Yanga SC kuvuna alama tatu zikisindikizwa na mabao matatu kwa moja.
Kwa matokeo hayo,wawakilishi hao wa Tanzania kwenye CAFCL wamefikisha alama nne baada ya mechi nne na kukwea mpaka nafasi ya tatu kwenye Kundi A wakiwa alama sawa na MC Alger waliopo nafasi ya pili.
Vilevile kupitia Kundi A ndiyo inashikilia msimamo kwa alama 9 baada ya mechi tatu na TP Mazembe inafunga mkia kwa alama mbili baada ya mechi.