DAR-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Hamis Mwinjuma akiongozana na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali,Gerson Msigwa wameshuhudia mchezo wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe.
Mchezo huo umefanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tarehe 4, Januari 2025 ambapo Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya mpinzani wake TP Mazembe.
Baada ya mchezo, Yanga imekabidhiwa kiasi cha shilingi milioni 15 ikiwa ni zawadi ya goli la Mama, kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ikilenga kuhamasisha maendeleo ya soka nchini.