NA DIRAMAKINI
KIUNGO wa kati wa Kimataifa wa Young Africans Sports Club (Yanga SC),Stephane Aziz Ki amerejesha matumaini ya klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Matumaini hayo yanakuja kuufuatia bao la dakika 7 ambalo liliwapa Yanga ushindi dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan katika dimba la Cheikha Ouldi Boidiya, Mauritania.
Kwa matokeo hayo ya Januari 12,2025 Yanga inahitaji ushindi wowote kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya MC Alger katika dimba la Benjamin Mkapa ili kufuzu hatua ya robo fainali ya CAFCL.
Yanga SC katika Kundi A lenye timu nne ipo nafasi ya tatu kwa alama saba baada ya mechi tano, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Al Hilal yenye alama 10 baada ya mechi tano.
Aidha, MC Alger wapo nafasi ya pili kwa alama nane baada ya mechi tano huku TP Mazembe ikiburuza mkia kwa alama 2 baada ya mechi tano.
Tags
Al Hilal Omdurman
Habari
Ligi ya Mabingwa barani Afrika
Michezo
Yanga SC
Young Africans Sports Club