DAR-Uongozi wa Young Africans Sports Club umetoapole kwa mchezaji wao Chadrack Boka, kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi kilichotokea Januari 11,2025 nyumbani kwao Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"Uongozi wa Young Africans unaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na unawataka wanafamilia wote kuwa na subira.
"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina,"imeeleza sehemu ya taarifa ya Yanga SC.