DAR-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeondolewa rasmi katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika.
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu NBC Tanzania waimeishia hatua ya 16 bora ya mashindano hayo baada kushika nafasi ya tatu kwenye kundi A.
Ni kufatia sare ya bila kufungana na MC Alger katika mchezo uliopigwa Januaria 18, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Yanga SC ilihitaji ushindi ili kufuzu kwa mara pili mfululizo hatua ya robo fainali,lakini mipango ya MC Alger ilifanikiwa kuwalazimisha sare nyumbani.