Zanzibar Heroes uso kwa uso na Burkinabe

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Burkinafaso katika michuano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup).

Mtanange huo utapigwa Januari 6,2025 majira ya saa 19:00 usiku ndani ya dimba la Gombani (Gombani Stadium) huko kisiwani Pemba.
Zanzibar Heroes itashuka dimbani ikiwa ina matokeo mazuri baada ya kuwachapa ndugu zao wa Kilimanjaro Stars bao 1-0.

Feisal Salum ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 51 ambapo mtanange huo ulipigwa hapo hapo Gombani Stadium siku ya Januari 3,2025.

Aidha,michuano ya mwaka huu ambayo imejumuisha timu za taifa badala ya klabu, imeanza kwa hekaheka nyingi kutokana na mabadiliko ya dakika za mwisho katika ratiba baada ya Uganda na Burundi kujiondoa.

Waandaaji wa michuano walilazimika kupangua ratiba, na hivyo mchezo wa ufunguzi kuwa kati ya ndugu wawili Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes.

Wakati huo huo, Januari 5,2025 timu ya Harambee Stars ya Kenya imetoka sare ya 1-1 katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Mapinduzi Cup 2025 inayoendelea Pemba, Zanzibar.

Kikosi cha kocha Francis Kimanzi kilikuwa zimesalia dakika chache kuandikisha ushindi kabla ya Burkina Faso kufunga bao la kuchelewa na kulazimisha sare ya bao moja kwa moja.

Aidha,baada ya kukosa nafasi kadhaa mbele ya lango, James Kinyanjui aliipatia Harambee Stars uongozi baada ya kupiga shuti lililorudishwa nyuma.

Mshambuliahi huyo wa KCB FC hakufanya makosa kupachika mpira wa adhabu uliopigwa na Boniface Muchiri ambao kipa wa Burkinabe aliupangua tena.

Kinyanjui alipiga mpira kurejea wavuni dakika nne katika kipindi cha nyongeza kabla ya muda kutamatika.

Kipindi cha pili Burkina Faso walifanya mabadiliko na kutengeneza nafasi za kufunga mabao bila mafanikio, ingawa mechi ilipokaribia kumalizika Aboubacar Traore aliisawazishia Burkina Faso dakika 90' ya mtanange huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news