ZANZIBAR-Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Soka (Zanzibar Heroes) imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 2-1 mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa Januari 13,2025 katika Uwanja wa Gombani Pemba.
Mabao ya Zanzibar Heroes yamefungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika 41 na Hassan Haji Ali (Cheda) dakika ya 90 huku bao pekee la Burkina Faso likifungwa na Aboubacar Traore dakika ya 70.
Wakati huo huo,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi ameialika Ikulu timu hiyo kwa chakula cha mchana Jumatano ya Januari 15,2025.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa mwaliko huo Uwanja wa Gombani Pemba baada ya timu hiyo kufanikiwa kulitwaa Kombe la Michuano ya Mapinduzi 2025.
Rais Dkt.Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi alikabidhi kombe kwa bingwa mabingwa hao wa Mapinduzi Cup 2025.