Zanzibar imevuka malengo ya Ilani ujenzi wa viwanja vya michezo-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ilieleza kufanyika ukarabati wa Uwanja wa Amani pekee, lakini Serikali imevuka malengo kwa viwanja vya wilaya na inalenga kujenga Academy kila mkoa.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la nsingi la ukarabati nkubwa wa Uwanja wa Gombani na viwanja vingine Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa hatua ya kuvikarabati viwanja vya New Amaan Complex, Mao Tse Tung na Gombani na ujenzi wa viwanja 17 kila wilaya unalenga kuibua vipaji nchi nzima katika ngazi zote.

Rais Dkt. Mwinyi amesema, umefika wakati kwa Zanzibar kuzalisha vipaji vya vijana watakaokuwa na uwezo wa kucheza nje ya nchi.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amefafanua kuwa,wachezaji wakubwa wanaotamba katika ligi za Uingereza, Hispania na Italia wametoka katika Academy za Soka katika nchi zao jambo alilolielezea kuwa ni lazima lifanyike Zanzibar.

Ameongeza kuwa, Serikali ininaweka mkazo katika ukarabati wa Uwanja wa New Amani Complex utumike ipasavyo katika Michuano ya CHAN itakayofanyika nchini mwezi wa Februari na Michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyika nwaka 2027 Tanzania ikiwa mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya.Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameitakia kila heri Timu ya Taifa ya Zanzibar )(ZANZIBAR HEROES) inayoshiriki Michuano ya Mapinduzi kufanya vema na kushinda Kombe hilo.

Uwanja wa Gombani unafanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo uwekaji wa paa jipya,ujenzi wa kuta,vyumba vya wachezaji,Eneo la Watu Mashuhuri, Maegesho,Tartan ,Uwekaji wa Minara, Mifumo ya Maji na Umeme pamoja na Ujenzi wa Uwanja wa Mazoezi pembezoni mwa Uwanja huo.
Ukarabati huo wa Awamu ya pli utagharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 4,250,000 unafanywa na Kampuni ya REFORM SPORTS ya Uturuki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news