Zuchu kuipeleka Wasafi Media mahakamani

DAR-Msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Masoud maarufu kwa jina la Zuchu ameandika barua kwenda kwa bosi wa Kituo cha Wasafi Media,Naseeb Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz) akilaumu kituo hicho kumfanyia udhalilishaji kupitia maudhui yao wanayoyatengeneza kwenye kipindi cha Mashamsham.
"Kwako kiongozi, kinachoendelea sasa mitandaoni kupitia maudhui ya kipindi chenu Mashamsham kimekuwa kama sehemu ya kuniumiza na kunididimiza kisanaa na kiafya ya nwili na akili. Lakini nasema nashukuru na nimeyapokea yote.

"Nimekuwa msanii wa taasisi mwenye kasi na mwenye kuipambania kazi yangu licha ya uwekezaji unaofanywa na kampuni yenu sikatai ni jambo kubwa na la kheri kumkomboa binti mwenye kipaji kwa kumuwekezea, lakini nauliza je, ni haki hicho kutumika kama silaha pia.

"Au niliwakosea nini mpaka kufikia kunifanyia bullying na harassment hizi. Nasibu, familia yako wanabaya langu lipi ambalo wanaona ni haki wao hata wakiwa na mahojiano binafsi kutokuweka stara ya mambo yangu, na huwa wanahakikisha hawakuharibii wewe bali mimi.

"Nimefikia hatua leo ninaandika barua ya kisheria kwa walezi wangu kwa sababu ya ukandamizaji wa mara kwa mara juu yangu.

"Inauma sana, nitaenda mahakamani na pengine sitaweza kushinda taasisi yenu yenye nguvu, lakini hata nikishindwa huko namuachia Mwenyezi Mungu yeye ndiye Hakimu wa mwisho.

"Asanteni ninashukuru kwa kuendelea kunibully na kuniharrass. Nilishaomba sana kwako kama kiongozi, lakini mara nyingi maombi yangu hugonga mwamba na kunatengenezwa content za kusudio la kunivunjia heshima, kuniumiza na kuharibu afya yangu ya akili.

"Mimi ni binti na mwanamuziki pia, sijawahi kuona media yoyote inani-harras kama ambavyo media ya taasisi yenu mmekuwa mkifanya.

"Sina cha kuwafanya kikubwa nyinyi ni wenye nguvu na mimi ninamshitakia Mwenye Ukuu, utukufu zaidi yangu na ninayenuamini zaidi Mwenyezi Mungu;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news