ZANZIBAR-Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar (BASSFU) limewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa maeneo ya sanaa na burudani kama vile kumbi za starehe, baa na maeneo ya hoteli kwamba zuio la upigaji wa muziki linaendelea.
Ni kufuatia kumalizika kwa ruhusa maalum iliyotolewa na Serikali katika kipindi cha Mkesha wa Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wa 2025.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo ikiwataka wamiliki wa maeneo ya sanaa na burudani kukamilisha utengenezaji wa maeneo ya kudhibiti sauti (soundproof) ili waweze kuruhusiwa kwa masharti maalum ya upigaji muziki.
"Hatua za kisheria zitaendela kuchukuliwa kwa mtu au taasisi yeyote itayokuti kana inafanya shughuli za sanaa na burudani kinyume na maelekezo ya Serikali.
"Maafisa wa baraza kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali zinaendelea na ziara za ukaguzi katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba."