MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR (ZURA) IMETANGAZA BEI MPYA YA UMEME KWA WATEJA WA HUDUMA HIYO INAYOTARAJIWA KUTUMIKA RASMI JANUARI 20, MWAKA HUU.
AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MENEJA UHUSIANO MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI ZANZIBAR ZURA MBARAKA HASSAN HAJI HUKO KATIKA OFISI ZA MAMKALA HIYO MAISARA.
AMESEMA, ZURA IMEPOKEA MAOMBI YA KUBADILISHA BEI YA UMEME KULIKOTOKANA NA MAHITAJI YA MABORESHO YA LAZIMA YA MIUNDOMBINU YA UMEME ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MABORESHO HAYO.
AKITAJA MABADILIKO HAYO MBARAKA AMEFAHAMISHA KUWA TOZO YA KUTOA HUDUMA (SAVES CHAGE) KWA MWEZI NI SHILINGI 2,100 KAMA ILIVYOKUWA HAPO AWALI.
AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA BEI HIZO ZIMETOA PUNGUZO LA TZS SHILINGI 190 KWA WATUMIAJI WADOGO WADOGO AMBAO WALIKUWA WAKILIPA TZS 480 KWA UNIT KILA WANAPOVUKA MATUMIZI YA UNITI 50 KWA MWEZI AMBAPO KWA SASA WATALIPA TZS 290 KWA UNIT.
HATA HUYO MBARAKA AMEBAINISHA KUWA MABADILIKO HAYO HAYATAHUSISHA TOZO ZA KUTOA HUDUMA ( SERVES CHARGE) NA BEI YA MAHITAJI YA JUU ( DEMAND CHARGE) ZITABAKI KAMA ZILIVYO.