KILIMANJARO-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema,Paul Sita (25) mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni dereva wa gari dogo, Exaud Mbise (65) na Apaikunda Ayo (61) wote wakazi wa Mkoa wa Arusha wamefariki katika ajali.
Ajali hiyo imetokea leo Februari Mosi,2025 majira ya saa 12:30 asubuhi katika eneo la Mdawi katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ikihusisha basi la kampuni Esther Luxury Coach na gari ndogo aina Toyota RAV 4.
Kamanda Maigwa amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari dogo kujaribu kuyapita magari mengine, bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na basi hilo la abiria.