DAR-Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Moses Daudi maarufu kama Shija (35) aliyekuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kwa tuhuma za unyang'anyi kwa kutumia silaha, ubakaji na ulawiti amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa kwa risasi.