DAR-Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC (Mzima Dabi) uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jiji Dar es Salaam umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Katika mchezo huo wa Februari 24,2025 Djibril Sillah aliipatia Azam bao la kwanza dakika ya kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Iddi Nado.
Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata maumivu dakika ya 20 na nafasi yake ikachukuliwa na Chamou Karaboue.
Elie Mpanzu aliwapatia Simba SC bao la kusawazisha dakika ya 25 baada ya kazi safi iliyofanywa na Kibu Denis aliyetoka na mpira nyuma na kuwazidi kasi walinzi wa Azam na kutoka pasi ya upendo.
Mlinzi wa kati Abdulrazack Hamza aliwapatia bao la pili kwa kichwa dakika 76 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Zidane Sereri aliisawazishia Azam bao hilo dakika ya 88 baada ya kumalizia mpira mrefu uliopigwa kutoka katikati ya uwanja na Feisal Salum.
Kwa matokeo hayo Simba SC inaendelea kubakia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania ikiwa na alama 51 baada ya mechi 20.
Aidha, watani zao Yanga SC wanaendelea kutamba kileleni mwa ligi kwa alama 55 baada ya mechi 21. Ufuatao ni msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara;