Aziz Ki amuoa rasmi Hamisa Mobetto

DAR-Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki amemuoa rasmi mwanamitindo Hamisa Mobetto katika hafla ya ndoa iliyofanyika leo, Februari 16, 2025 katika Msikiti wa Masjid Nnuur, Mbweni jijini Dar es Salaam.
Ndoa hiyo imefungwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar akisaidiana na jopo la masheikh wengine.
Akizungumza baada ya ndoa, Sheikh Walid aliwatakia wanandoa hao maisha mema na kuhimiza jamii kuepuka zinaa.
Sherehe rasmi ya ndoa hiyo inatarajiwa kufanyika Februari 19, 2025, katika ukumbi wa Superdome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Februari 15,2025 Aziz Ki alilipa mahari ya ng’ombe 30 na shilingi milioni 30, mahari iliyokabidhiwa kwa familia ya bibi harusi na Rais wa Yanga, Mhandisi Heris Said kwa niaba ya bwana harusi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news