MORONI-Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu leo amekutana na mtangazaji mkongwe wa Sauti ya Ujerumani Bi.Ummulkheir Hamidou ambaye ni mtanzania mwenye asili ya Comoro.

Bi Ummulkheir ambaye anakumbukwa kwa sauti yake nzito redioni na kiswahili fasaha,ameridhia ombi la ubalozi la kushirikiana nae katika kukuza Kiswahili nchini Comoro na kueleza namna anavyoona umuhimu wa Kiswahili nchini Comoro.

Bi Ummulkheir amekuwa mtangazaji wa Sauti ya Ujerumani kuanzia mwaka 1979 hadi 2020 alipostaafu rasmi.Ametembelea Ubalozini leo akiambatana na mumewe Bwana Hamidou Ali.