Benki Kuu haijatoa leseni wala kuruhusu shughuli za LBL
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapenda kuutaarifu umma kuwa, haijafanya mazungumzo wala kutoa maelekezo yoyote ya kupewa leseni au kuruhusiwa kwa kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL), tofauti na taarifa mbalimbali zinazosambaa mitandaoni.