Biashara saa 24 Kariakoo

DAR-Wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo lililopo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mkoani Dar es Salaam wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24 kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Albert Chalamila ameyasema hayo Februari 24,2025 kwa nyakati tofauti akiwa katika Studio za Crown Media na Kariakoo akiwa anaongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.

RC Chalamila amesema, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Februari 25,2025 mpaka kilele chake Februari 27,2025..."tunautangazia umma kuanza rasmi kwa biashara saa 24 ambapo Kariakoo ni eneo la uzinduzi lakini wilaya nazo zitaendelea kufanya hivyo katika maeneo yao ili kuweza kurasimisha biashara saa 24."

Aidha,RC Chalamila amesema, mataifa yaliyoendelea hufanya biashara saa 24 ambayo hupanua wigo wa ajira kwa vijana, lakini pia kuongezeka kwa kodi hivyo kwa kuwa Mkoa huu ni kitovu cha Biashara kwa kufanya hivyo vijana watapata fursa za kujiajiri na TRA pia itaweza kukusanya mapato mengi zaidi

Sambamba na hilo RC Chalamila amewahakikishia wafanyabiashara usalama wa kutosha wasiwe na shaka Dar es Salaam ni salama sana miundombinu ya kiusalama inaendelea kuimarishwa ikiwemo kuwekwa taa na Camera katika Mitaa.

Vilevile RC Chalamila amesema baada ya uzinduzi huo anatarajia kuunda kamati itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kwa ajiri ya kupitia sheria zinazokinzana na kufanya biashara saa 24 hasa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri za Manispaa.

Mwisho wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kufanya biashara saa 24 kwa kuwa unafaida kubwa kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news