ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,Serikali imefanya juhudi maalum za kuhakikisha bidhaa za vyakula zinakuwepo za kutosha wakati wa Ramadhani.
Alhaj Dkt. Mwinyi amesema hayo alipozungumza katika Kongamano la Kumi la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Amesema kuwa, Serikali imeandaa mazingira wezeshi ya uingizaji wa bidhaa hizo hapa nchini.
Halikadhalika, Dkt.Mwinyi ameendelea kuwahimiza wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa wakati wa Ramadhani pamoja na kufuata bei elekezi ili kuwapa unafuu wananchi kumudu kununua.
Akizungumzia suala la amani wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu amewasisitiza wanasiasa,viongozi wa dini na waandishi wa habari kupaza sauti zao kuhubiri amani ili nchi iendelee kuwa na utulivu.