KILIMANJARO-Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Mpanda wamefika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujifunza mbinu bora za uendeshaji wa mamlaka za maji.
Takribani watumishi 15 wamezuru Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) kujionea utekelezaji wa miradi ya maji na uendeshaji wa mamlaka.
Akizungumza wakati akipokea ugeni huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA),Mhandisi Kija Limbe amebainisha mambo muhimu yanayochangamsha utendaji kazi wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mpanda,ndugu Martin Mwakabende na Kaimu Mkurugenzi wake, Rehema Nelson wameeleza lengo la ziara yao.Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,ndugu Albert Msovera amesema, MUWSA ni miongoni mwa mamlaka za kuigwa na ndio maana wametembelea ili kukuza ubunifu na utendaji kazi miongoni mwa watumishi wao.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI KWA KINA;