KAZAKHSTAN-Bondia Abedi Zugo atandikwa kwa TKO katika pambano liliofanyika usiku wa jana kuamkia leo nchini Kazakhstan.
Zugo kutoka Tanzania amekutana kichapo hiko katika raundi ya tatu kutoka kwa bondia Bekman Soilybaev wa Kazakhstan kwenye pambano la raundi la raundi 12 na kushindwa kuendelea kupigana.
Kufuatia ushindi huo kumemfanya bondia Soilybaev kuwa bingwa wa Dunia wa mkanda wa UBO baada ya pambano hilo ambalo limefanyika nchini Kazakhstan katika eneo la Aktau humo kwenye ukumbi wa Halyk Arena sport complex.
Soilybaev ni bondia mwenye hadhi ya nyota nne namba namba 27 Duniani kati ya mabondia 1957 pia ni namba mbili nchini kwao kati ya mabondia sita katika uzani wa Super feather akiwa amecheza mapambano 21 akishinda 20 huku 11 kati ya hayo yakiwa kwa 'KO' na akipoteza pambano moja pekee kwa 'points'.
Kwa upande wake Zugo ni bondia mwenye hadhi ya nyota tatu akiwa namba 67 Duniani kati ya mabondia 1957 na nchini Tanzania ni wa pili kati ya mabondia 87.
Zugo amecheza mapambano 16 akishinda 15 na 13 kati ya hayo akishinda kwa 'KO' na kupoteza moja.
Mara ya mwisho Zugo kupoteza pambano kabla ya kupigwa na Soilybaev ilikua julai 20, 2024 alipopigwa kwa 'KO' na bondia Albert Kimario katika pambano lililofanyika jijini Mbeya na baadae taarifa zikatoka kuwa halikua pambano rasmi bali lilikua ni la maonesho.