DAR-Bondia wa ngumi za kulipwa Kennedy Ayo amebakiza siku 10 ili kwenda nchini Uganda kupigana pambano lake la kimataifa la uzani wa.
Ayo ambaye ni mdogo wake na Juma Ayo mtangazaji wa Crown Media, anaenda kucheza pambano lake la pili la kimataifa baada ya lile la mwisho aliloshinda nchini Urusi dhidi ya mpinzani wake Ismat Guliyev lililofanyika Disemba 13, 2024.
Ayo ataenda Uganda kupigana na Henry Kigongo ambaye ni raia wa nchi hiyo katika pambano la raundi 10 la uzani wa 'welter' ambapo pambano litafanyika Februari 28, 2025 kwenye ukumbi klabu ya mchezo wa ngumi uliopo katika eneo la Kulambiro.
Ayo ni bondia namba sita nchini Tanzania kati ya mabondia 53 na Duniani ni wa 286 kati ya 1973 akiwa na nyota moja na nusu katika uzani wa 'middle' huku akicheza mapambano nane akishinda sita kati ya hayo ameshinda mawili kwa 'KO' na kupoteza mawili ambayo yote amepigwa kwa 'KO'.
Naye Kigongo ambaye ni mpinzani wa Ayo ni bondia namba 2 nchini Uganda kati ya mabondia 28 na Duniani ni wa 113 kati ya 2458 akiwa na nyota mbili na nusu katika uzani wa 'welter'.
Ikumbukwe pambano la mwisho la Kigongo lilikua ni Novemba 24, 2024 ambapo alimpiga bondia wa Tanzania Issa Maneva kwa 'points' pia bondia huyo wa Uganda aliwahi kumpiga Cosmas Cheka kwa 'TKO' nchini humo mnamo Novemba 11, 2023.
Kila la la kheri bondia Ayo nenda kafute uteja wa mabondia wa Tanzania kwa kupigwa na Kigongo pia kaipeperushe vyema bendera ya Tanzania kwa upande wa mchezo wa ngumi za kulipwa.