Bondia Mtango akisa visa kwenda kupigana Ubeligiji

DAR-Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Salim Jengo almaarufu Mtango siku ya jana ameshindwa kupanda ulingoni kucheza pambano la kimataifa la ubingwa nchini Ubeligiji.
Mtango ilibidi acheze pambano hilo la raundi 10 la ubingwa wa mabara wa IBO (International Boxing Organization Intercontinental Super Lightweight) dhidi ya bondia Hovhannes Martirosyan mwenye uraia pacha wa nchini Ubeligiji na Armenia.

Lakini pambano hilo limeshindwa kufanyika baada ya Mtango kuchelewa kupata viza ya kusafiria kwenda nchini Ubeligiji na siku ya jana mpinzani wake Martirosyan alipewa mpinzani mwingine aliyetambulika kwa jina la Victor Enrique Julio Perez raia wa Colombia.

Kufuatia kukosekana kwa Mtango kulitoa fursa kwa Martirosyan na mpinzani wake Perez kupima uzito na kucheza pambano la kimataifa la raundi 10 lisilo la bingwa kwenye uzani wa 'Super Lightweight' lililo fanyika kwenye ukumbi wa Hasselt jijini Limburg nchini Ubeligiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news