ZANZIBAR-Balozi wa Heshima wa Brazil Visiwani Zanzibar,Abdulsamad Abdurahim amesema, nchi ya Brazil imekusudia kutoa mafunzo kwa Askari Polisi ili kuwajenga na kuwaweka tayari kudhibiti na kufanya uokozi kwa njia ya amani katika mikusanyiko mikubwa.
Akizungumza katika ziara ya Balozi huyo pamoja na Maafisa kutoka Brazil, Febuari 16,2025 Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amesema ziara na mafunzo watakayotoa yanalenga kukuza ushirikano baina ya nchi hizo.