CAIRO-Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF EXCOM) imefanya marejeo ya kanuni za usajili na sasa mchezaji aliyetumiwa na timu A anaweza kucheza timu B akisajiliwa kwenye dirisha dogo ndani ya msimu mmoja wa mashindano.
Pia,kamati imeamua kusogeza mbele dirisha la usajili la CAF hadi kuwa Februari 28 badala ya Januari 31,2025.
Marekebisho hayo yameziangazia pia timu zinazokwenda kushiriki Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu yatakayofanyika Juni,2025 huko Marekani.