DODOMA-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kimeandaa mpango wa kuanza kutoa mafunzo ya uandishi wa habari za michezo chuoni hapo.

Aidha, Waziri Kabudi amesema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni moja na Milioni Mia Tano (1,500,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho kilichopo Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.